WATUMISHI WA HOSPITALI MKOANI KATAVI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA YUMO MWANANCHI ALIYESAHWISHI KUTOA SHILINGI 500

Na.Issack Gerald-Katavi
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Mkoani Katavi imewafikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Katavi watuhumiwa watatu  wakiwemo  watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.
Kwa Mjibu wa taarifa ya Mkuu wa Takukuru Mkoani Katavi John Minyenya kwa vyombo vya habari,amewataja wauguzi wa Hospitali hiyo waliofikishwa mahakamani kuwa ni Yohana Paul Deo(25) mkazi wa Kawajense anayetuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 40,000 kutoka kwa mwananchi aliyekuwa akimuuguza mgonjwa wake baada ya kupata ajali ya pikipiki na kuvunjika mguu na mkono.
Deo katika kesi hii,anadaiwa kuomba fedha hiyo Septemba 22 mwaka huu ili amsaidie ndugu wa mgonjwa huyo kupatiwa huduma baada ya kukaa siku mbili hospitalini hapo bila kuhudumiwa.
Muuguzi mwingine ambaye amefikishwa mahakamani ni Marco Bunduki James(31) mkazi wa Kawajense ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 30,000 Oktoba 07 mwaka huu kutoka kwa mwananchi aliyekuwa akimuuguza mwanaye ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya kuvunjika mguu alipokuwa akicheza mpira wa miguu.
Kwa taarifa ya Takukuru ni kuwa Mtuhumiwa anadaiwa kuomba rushwa ili amsiadie ndugu wa mdonjwa huyo kumfunga POP huku mshtakiwa wa tatu akiwa ni Evaristi Juma Lusaba(27) Mkazi wa Itenka aanayeshtakiwa kwa kosa  kumshawishi kumpatia mlinzi wa hospitali ya Wilaya ya Mpanda shilingi 500 ili mlinzi huyo amruhusu mananchi huyo kuingia wodini kumpelekea mgonjwa soda katika muda ambao siyo wa kuona wagonjwa huku akidaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 13 mwaka huu.
Watuhumiwa wote wanatuhumiwa kwa makosa ya kushawishi,kuomba na kupokea rshwa kinyume kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Kaufuatia matukio hayo,Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Katavi imetoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na vitendo vya rushwa huku taarifa ikionesha kukamatwa kwa wathumiwa hao kumetokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya wananchi na taasisi hiyo.
Takukuru imekuwa ikisisitiza kutunza siri za yeyote anayeripoti taarifa za wanaoomba na kupokea rushwa.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA