RAIS MAGUFULI,KENYATTA,NKURUNZIZA,IDRISI,MAHAKAMA YA KENYA NA JSEHI LA ZIMBABWE WATUNUKIWA TUZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe
Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa
kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Rais Magufuli mwenye miwani katika picha |
Marais wengine ambao wamepata tuzo ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye
amejishindia tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia
nchini Kenya.
Mahakama
ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela
Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.
Rais wa Taasisi ya Mandela,Dk
Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa
kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa
mamlaka.
Mahakama ya Juu ya Kenya
ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa
ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka
mshindi.
Rais wa
Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana
na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Rais wa
Burundi, Pierre Nkurunziza akituzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).
Chanzo:Mwananchi
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments