JESHI LA POLISI ZANZIBAR LAAMUA KUJITATHMIN
Jeshi la Polisi Zanzibar,limeamua kujitathmini kwa lengo la
kusahihisha kasoro watakazobaini ili kutoa huduma bora kwa jamii.
Mpango huo wa kujitathmini unafanyika kwa utaratibu wa
kusikiliza maoni na ushauri kutoka kwa wananchi,wakilenga zaidi kujenga imani
ya raia kwa jeshi hilo.
Utaratibu huo wa kujitathmini ulitangazwa na Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis Ahmed kuwa wameamua kufanya hivyo kwa
lengo la kuliweka jeshi karibu na jamii na kufanya kazi pamoja ya kupambana na
vitendo uhalifu.
Huu ni utaratibu mzuri wa kufanya mawasiliano na raia ambao
unafaa kuendelezwa kwa maeneo yote ya visiwa vya Unguja na Pemba ambapo
imeelezwa kuwa utaratibu huu utaondoa au kupunguza kwa kiasi kikubwa uadui au
hofu iliyojengeka kati ya raia na polisi.
Aidha ni nafasi nzuri kwa maofisa wa Jeshi la Polisi
kuwaelimisha raia na kuwaeleza dosari wanazoziona katika jamii katika kupambana
na vitendo vya uhaifu na kuwatia hatiani wanaofanya vitendo hivyo.
Chanzo:Zanzibar24
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments