MAREKANI YAWAWEKEA VIKWAZO WATAALAMU WA MAKOMBORA KOREA KASKAZINI
Marekani imewawekea vikwazo maafisa wawili wa Korea
Kaskazini akidai wamechangia kuundwa makombora ya nchi hiyo.
Wizara
ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na kusema kuwa
wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya masafa marefu wa
Korea Kaskazini.
Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa
liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake
ya makombora ya masafa marefu huku Korea Kaskazini ikisema kwa hatua hiyo ni
kama ya vita.
Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia
shughuli zozote za wanaume hao wawili zinazofanywa nchini Marekani na hata
kutwaliwa kwa mali yao zilizo nchini Marekani.
Wanaume
hao wawili wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim
Jong-un wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora.
Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora
tofauti ambayo Korea Kaskazini inasema yanaweza kufika nchini Marekani.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments