WILAYA YA MPANDA KUANZISHA KILIMO ZAO LA PAMBA NA KOROSHO-Oktoba 6,2017
Na.Issack
Gerald-Mpanda Katavi
Pamba |
Korosho |
Matinga amebainisha hatua hiyo wakati akizungumza kuhusu uanzishwaji wa mazao mbadala ya kibiashara Mkoani Katavi.
Amesema jumla ya hekta 1236
zinatarajiwa kulimwa katika msimu wa kilimo mwaka 2017/2018 ambapo mpaka sasa
wakulima wapatao 639 wamejiandikisha kuanza kulima zao hilo huku matarajio ikiwa
ni kuvuna tani mbili hadi tatu.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017
wakulima wapatao 68 walilima zao hilo na kuvuna tani 35 zilizouzwa wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga ambapo msim.
Amesema kata tatu za Ugalla,Mtapenda
na Nsimbo za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kati ya kata 12 za Halmashauri
hiyo ndizo ambazo zimechaguliwa kuanzisha kilimo cha zao hilo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Lilian
Matinga amesema wanafanya utafiti kuhusu zao la korosho ambapo mpaka sasa
wamesia mbegu za korosho kilogramu kumi kwa ajili ya kuanza kulima zao hilo kwa
mwaka huu.
Mwezi uliopita,Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa kumi akiwemo
mkuu wa Mkoa wa Katavi kuanzisha kilimo cha zao la pamba kwa ajili ya
kutekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments