GODBLESS LEMA : KAMA SERIKALI YA MAGUFULI HAIJUI NANI ANAEFANYA MATUKIO YA MAUAJI, BASI NAE HAYUKO SALAMA-Oktoba 6,2017
Godbless Lema akizungumza(mwenye shati (jeupe) na waandishi wa habari |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimehoji maswali mbalimbali kwa
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP),Simon
Sirro kuhusu mambo yanayoendelea kwenye upelelezi wa Ben Saanane,Tundu Lissu na
aliyemtishia Mbunge wa Mtama,Nape Nnauye.
Akizungumza
katika mkutano na wandishi wa habari Waziri kivuli wa mambo ya ndani na mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema,amewahoji viongozi hao,namna amabavyo wamekuwa
wakishughulikia masuala yanayohatarisha usalama wa nchi.
Katika
mkutano huo mh Lema amesema swala la usalama wa nchi na maisha ya kila
mtanzania yanamuhusu kila mmoja hapa nchini hususani waandishi wa habari.
‘’Tuna IGP anaefikiri kuwa kamanda mkakamavu
ni kubeba siraha,na mimi nataka nimwambie siro huwezi kuprove kwamba wewe ni
kamanda kwa sababu umezungukwa na watu wenye bunduki,utaprove kwamba wewe ni
kamanda kama unaweza ukacary on the truth, “amesema mh, lema”
Mh,lema
amesema kuwa wananchi wameendelea kupoteza matumaini na jeshi la polisi
kutokana hilo kutokuchukua hatua haraka katika baadhi ya matukio amabyo
yameendelea kutokea hapa nchini.
Aidha
amesema yeye yupo kwenye tageti ya kuuwawa kwa kuwa kilichotokea kwa mh lisu ni
mwendelezo wa mambo mengi yanaoweza kutokea kwa viongozi wao.
Katika
hatua nyingine amesema ofisi ya
IGP,idara ya usalama wa taifa,pamoja na waziri wa mambo ya ndani wao kama
hawajui watuhumiwa na kusema ni watu wasiojulikana,kama waziri anasema kuna
watu wasiojulika basi waziri hatakiwi kujulikana kama yupo ofsini.
Hata
hivyo mh Lema amesema rais magufuli ajue kuwa wao wanamwili,wanadamu na pia
wanandugu,na kama serikali ya magufuli haijui nani anaefanya matukio hayo basi
yeye mwenye hayuko salama,na kama yeye mwenye hayupo salama kwa nini
ameyanamazia?.huku akinukuu maneno ya biblia, uwa kama ilivyoandikwa
yanayofanyika dalini yatasitirika hadharani,ambapo amesema hivi karibuni mambo
yote yatasitirika hadharani.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments