UNGUJA ZANZIBAR:KILIMO CHA ASILI NI KIVUTIO NJE YA NCHI-Oktoba 6,2017
IMEELEZWA kuwa kilimo cha asili kisichotumia kemikali ni kivutio
kwa idadi kubwa nchi za nje kuthamini ubora wa bidhaa za Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa bodi kutoka Jumuia ya
wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima Ahmed Saleh
Mbarouk wakati akizungumza na Maisha fm radio.
Amesema kutokana na ubora wa kilimo cha mboga mboga
kinacholimwa Zanzibar ni
vyema wakulima kuendeleza kilimo hicho ili kuongeza kasi ya biashara za nje ya
nchi.
Mjumbe huyo amefahamisha kuwa suala la kusarifu vyakula kutaweza
kupunguza wimbi la matunda kuharibika wakati wa mavuno sambamba na kusubiri
soko na kuongeza pato la wakulima.
Aidha ameziomba taasisi kuwa na ubunifu wa kuwawezesha wakulima
kuwapatia nyezo za kusarifia mazao ili kumuwezesha mkulima kuwa na kilimo
chenye tija.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au
P5Tanzania Limited Group
Comments