MANISPAA YA MPANDA WAIBUKA NA MASTA PLAN YA MPANGO MJI,MKUU WA MKOA WA KATAVI ATOA NENO-Oktoba 6,2017
Na.Issack
Gerald-Mpanda Katavi
Jengo la Ofisi za Manispaa ya Mpanda na Mkuu wa Mkoa |
Muhuga
ametoa kauli hiyo leo katika kikao cha
wadau wa Mpango Kabambe (Master Plan) kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa
ya Mpanda ambapo amesema lengo kubwa la Mkoa ni kuwa na mji uliopangika vizuri lakini
kuna baadhi ya watu wamekuwa wakikwamisha.
Aidha
amewataka viongozi wa mitaa pamoja na Kata
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wa Mpango huo ili wafanye kazi vizuri
sambamba na kuwashirikisha wananchi.
Kwa
upande wake Afisa Mipango Miji Mshauri kutoka City Plan Consultants LTD ya Dar
es salaam Bw.Iddy Mwerangi amesema,Mpango kabambe una majukumu mengi ikiwemo kupitia
mipango ya maendeleo iliyopo na kufanya utekelezaji wake pamoja na Kutoa mapendekezo yanayokidhi matakwa ya
kisheria.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bi.Enelia Lutungulu amewasistiza
viongozi kuwahamasisha wananchi ili mpango uende vizuri.
Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda ni miongoni mwa halmashauri hapa nchini zinazotekeleza
miradi inayofadhiliwa na benki ya dunia ambapo pamoja na Miradi mingine Halmashauri
ya manispaa ya Mpanda inaandaa mpango kabambe maarufu kama Master Plan utakaoongoza
matumizi ya ardhi ya manispaa ya Mpanda kwa kipindi miaka 20 ijayo.
Mpango
mchakato huo uliokuwa umeanza tangu mwaka 2010, haukufika mwisho kwa sababu ya
ongezeko la mahitaji ikiwa ni pamoja na ongezeko la ukubwa wa eneo la kiutawala
manispaa ya Mpanda hivyo kupelekea kuanza upya Mchakao huo kwa kuwa taarifa za
awali za msingi zilipitwa na muda wake.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments