WAZIRI LUKUVI MKOANI RUKWA NA MASUAL AYA MIGOGORO YA ARDHI
Uzembe
na utendaji kazi wa kimazoea kwa baadhi ya watendaji wa serikali wakati wa
ubinafsishaji wa shamba la Mlonje Dafco lenye ukubwa wa hekta 10,000 na kumpa
mwekezaji Tasisiya Efatha Ministry umewagharimu wananchi na kuibua migogoro ya
mara kwa mara baina ya mwekezaji huyo na vijiji jirani vinavyozunguka shamba
hilo.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi amesema hayo leo mjini
Sumbawanga wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali ngazi ya mkoa,
na halmashauri za wilaya ya Sumbawanga mjini na vijijini, wakiwemo wabunge wa
majimbo ya Kwela na Sumbawanga mjini.
Uzembe huo umesababisha serikali kukirimakosa
katika zoezi zima la kubinafsisha Shamba hilo hali iliyosababisha mgogoro huo
kushindwa kutatuliwa kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa RDC mjini hapa, Waziri Lukuvi alisema kwamba mwekezaji huyo
anapaswa kuachwa ili kuendelea na shughuli zake kwa kuwa shamba hilo alipewa
kihalali kwani waliofanya makosa wakati wakibinafsisha kwa mwekezaji ni
watendaji wa serikali ambao walifanya hivyo pasipo kufuata maelekezo ya
serikali.
Alisema njia pekee ya kutatua tatizo la baadhi ya vijiji
kikiwemo cha sikaungu ambacho wananchi wake wanalalamika kukosa radhi kwa ajili
ya shughuli za kilimo ni wizara kufanya mazungumzo na mmliki wa shamba hilo na
kuomba atoe ardhi kidogo kwa kijiji hicho.
Alisema iwapo wataafikiana itawalazimu wizara kupitia upya
michora ya hati yake na kugawa sehemu ya ardhi hiyo kwa kijiji hicho hali
ambayo itafanya na yeye aweze kufanya shughuli za uwekezaji pasipo kuingilia na
mtu yeyeto hivyo uwekezaji wake kuleta tija tofauti na ilivyo sasa ambapo
amekuwa akikabiliana na changamoto za migogoro kadhaa.
Mgogoro wa Shamba la Dafco Malonje umedumu kwa zaidi ya miaka
tisa sasa, ambapo iliuzwa kwa mwekezaji huyo mwaka 2008 na uongozi wa Manispaa
ya Sumbawanga kwa maelekezo ya uongozi wa mkoa wa Rukwa, kwa bei ya milioni Sh
600,000,000.
Awali,Mbunge wa Sumbawanga mjini,Aeshi Hilaly akizungumza katika
kikao hicho aliomba serikali itakapofanya mazungumzo na mwekezaji huyo kuhusu
kupitia upya mipaka iweze kumshawishi ili atoe ardhi kwa vijiji vyote 24
vinavyozunguka shamba hilo hali ambayo itasaidia kumaliza migogoro ya ardhi.
Mkuu wa mkoa huo, Zelothe Steven aliwataka wananchi wa vijiji
vinavyozunguka shamba hilo kuelewa kwamba serikali ipo kwa ajili ya kutatua
matatizo yao hivo sasa wanapaswa kuwa watulivu na kujitojiingiza katika vitendo
vya uvunjifu wa amani kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na watachukuliwa
hatua stahiki ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5tanzania Limited
Comments