BARAZA LA MITITHANI LATANGAZA MATOKEO DARASA LA SABA
Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza
matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu
umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa
NECTA Dkt. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950
waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama
250 ambazo walitakiwa kupata.
Dkt. Msonde ameendelea kusema kwamba kati ya
waliofaulu wasichana ni 341 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321,
015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na
asilimia 72.76%.
Katibu Mkuu huyo aliendelea kwa kusema kwamba
ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya
4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa
ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.
Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde
amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St.Peters-Kagera,
St,Severine-Kagera,
Alliance–Mwanza
Sir.John–Tanga
Palikas–Shinyanga
Mwanga–Kagera
Hazina-Dar es salaam
St,Severine-Kagera,
Alliance–Mwanza
Sir.John–Tanga
Palikas–Shinyanga
Mwanga–Kagera
Hazina-Dar es salaam
St. Anne Marie - Dar es salaam
Rweikiza – Kagera
Martin Luther - Dodoma.
Pia Dkt. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya
vibaya kitaifa ambazo ni
Nyahaa – Singida
Bosha – Tanga
Ntalasha – Tabora
Kishangazi – Tanga
Mntamba – Singida
Ikolo – Singida
Kamwala – Songwe
Kibutuka – Lindi
Mkulumanzi – Tanga
Kitwai A – Manyara
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5tanzania Limited
Comments