RAIS MAGUFULI ATUMA SALAAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA ASKOFU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tercisius
Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi
Mhashamu Castory Msemwa, kilichotokea jana tarehe 19 Oktoba, 2017 nchini Oman.
Mhashamu Askofu
Castory Msemwa amefariki dunia Mjini Muscat akiwa safarini kuelekea nchini
India kwa Matibabu.
Mhe. Rais
Magufuli amemuomba Rais wa TEC Mhashamu Tercisius Ngalalekumtwa kumfikishia
pole nyingi kwa Maaskofu wote wa TEC, Mapadre, Makatekista na waumini wote wa
Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi kwa msiba huu mkubwa uliotokea na amesema
anaungana nao katika kipindi cha majonzi na maombi kwa Marehemu.
Comments