TPA MKOANI RUKWA IMETOA MSAA WA SHUKA 1245 KATIKA IDARA YA AFYA
MAMLAKA ya bandari nchini(TPA) imetoa msaada wa
mashuka 1245 yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa halmashauri ya wailaya ya
Nkasi kwaajili ya idara ya afya wilayani humo.
Mkurugenzi wa bandari nchini Desderius Kakoko alisema kuwa msaada huo wanatoa katika halmashauri ambazo zina bandari kote nchini ikiwa ni sehemu ya kutoa ahasante wa halmashauri hizo.
Mkurugenzi wa bandari nchini Desderius Kakoko alisema kuwa msaada huo wanatoa katika halmashauri ambazo zina bandari kote nchini ikiwa ni sehemu ya kutoa ahasante wa halmashauri hizo.
Alisema kuwa mamala ya bandari nchini inachangia nusu ya
makusanyo ya taifa kwa mwezi ambayo ni shilingi bilioni Mia 5.5 ambapo
inatumika katika matumizi ya serikali.
Kakoko alisema kuwa kutokana na wilaya ya Nkasi kuwa na mahitaji
katika idara ya afya mamlaka hiyo imeamua kuchangia mashuka ikiwa ni katika
jitihada za kupunguza matatizo kwa wananchi.
Alisema nchi ya tanzania inapakana na nchi nane ambazo hazina
bandari nazinategemea bandari zilizopo hapa nchini hivyo basi nifursa nzuri ya
kuhakikisha kuwa uchumi unakua nakuongeza pato la taifa.
Akishukuru kwa msaada huo mbunge jimbo la Nkasi Kaskazini Ally
Kessy alisema kuwa msaada huo umekuja katika wakati muafaka kwani sekta ya afya
wilayani humo bado inamahitaji makubwa.
Alisema kuwa msaada huo sio mara ya kwanza kwa wilaya hiyo kwani
mamlaka ya bandari iliwahi kutoa msaada wa shilingi milioni 40 taslimu
kwaajili ya kusaidia sekta ya elimu na afya.
Hata hivyo aliisihi mamlaka ya bandari nchini kuhakikisha
inakuamakini na upande wa Zanzibar kwani kuna bandari bubu nyingi
zinazoikosesha serikali mapato.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5tanzania Limited
Comments