SERIKALI KUSHGHULIKIA HAKI ZA WALIMU
SERIKALI imesemna itaendelea
kushughulikia haki za walimu pamoja na kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili walimu ikiwa ni pamoja na kushirikiana na chama cha walimu
Tanzania ili walimu waendelee kufanya kazi katika mazingira rafiki kwa manufaa
yao na taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe
Muhando kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael
Muhuga aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa chama cha walimu
Tanzania CWT wilayani Mpanda mkutano ambao umefanyika katika ukumbi wa shule ya
sekondari St.Mary’s Mpanda.
Awali akisoma taarifa ya chama kwa
mgeni rasmi,katibu wa chama cha walimu Tanzania Wilayani Mpanda Wilison
Masolwa,pamoja na mambo mengine amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii kukata na kuchelewesha malipo kwa walimu
wastaafu suala ambalo wameiomba serikali kusimimia haki hizo ili kuhakikisha
mwalimu anapata haki zake kwa wakati.
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya
utendaji wa CWT Taifa Bw.Hamis Ismail akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wa
Chama cha Walimu Taifa amesema pamoja na mafanikio ya kuanzisha benki ya
mwalimu,kuanzisha ujenzi wa Ofisi za CWT Mkoa wa Katavi na kumtetea
mwalimu,amewataka walimu kusimama na kutetea chama chao.
Wakati huo huo chama kimewapatia bati
40 walimu wawili wastaafu Aloyce Kapinga na Mrisho Kinanda bati zenye thamani ya shilingi laki 680,000
pamoja na Shule ya Sekondari Mpanda Ndogo kupewa mifuko 5 ya simenti na 7 upande
wa shule ya Msingi Mpanda kama mchango
wa ujenzi wa vyoo shuleni suala ambalo limepongezwa na waliopatiwa mchango huo.
Kwa mjibu wa utawala wa chama cha
walimu Tanzania,Wilaya ya Mpanda inaundwa na Halmashauri mbili ambazo ni
Mpanispaa ya Mpanda iliyopo wilayani Mpanda na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
iliyopo wilayani Tanganyika ambapo katika mkutano huo uliokuwa umehudhuriwa na
wanachama karibu 200 ulikuwa ukiwashirikisha pia wakuu wa
wilaya,wakurugenzi,wawakilishi wa mifuko ya hifadhi,wataalamu wa idara katika
Halmashauri na taasisi za kifedha.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5tanzania Limited
Comments