WASAFIRI KUTOKA KATAVI,TABORA NA KIGOMA WANAOTUMIA TRENI YA RELI YA KATI KUONGEZEWA BEHEWA KURAHISISHA USAFIRI
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama- Katavi
SERIKALI imewahakikishia wakazi wa
mikoa ya Katavi,Tabora na Kigoma kuwa itaongeza mabehewa ya abiria na mizingo
katika treni ya reli ya kati ili kuruhusu abiria wengi kusafiri na
kusafirisha mizigo yao kuwa wasafiri
wengi wanatumia usafiri wa treni.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Makame Mbarawa mara baada ya kuhitimisha ziara ya ukaguzi wa reli na
miundombinu ya Mkoani Tabora.
Baadhi ya wakazi Mkoani Katavi
wamesema kuwa hatua hiyo ya serikali itarahisisha usafiri kwa wananchi.
Treni ya reli ya kati imeonekana
ikisafiri mara kwa mara kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma baada ya serikali kuongeza behewa hivi
karibuni.
Endelea kuwa name kufahamu kitakachojili kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments