BARAZA LA MADIWANI WILAYANI TANGANYIKA LAIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA MIRADI VIPORO YA MAENDELEO ILI WANANCHI KUENDELEA KUWA NA IMANI NA SERIKALI.
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Tanganyika
Katavi
BARAZA la madiwani Halmshauri ya
Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,limeiomba serikali
kuhakikisha inakamilisha miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali ili
kuwanufaisha wananchi kiuchumi na kimaendeleo.
Madiwani wa Baraza la madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda wakiwa katika kikao(PICHA NA.Issack Gerald) |
Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald) |
Baraza limetoa ombi hilo katika kikao
chake ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda
uliopo Mpanda Mjini.
Wamesema kuwa kukamilika kwa miradi
kutapelekea wananchi kuwa na imani kwa serikali yao katika kuwaletea maendeleo
huku madiwani wa baraza hilo wakitaka kutoibuliwa miradi mipya kabla ya
kukamilisha miradi viporo.
Katika kujibu hoja za madiwani wa
Baraza hilo,Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw. Ngalinda Hawamu Ahmada
amesema,serikali itaendelea kukamilisha miradi viporo iliyokwishaibuliwa ikiwa
ni sambamba na kuanzisha miradi mipya ya maendeleo.
Katika hatua nyingine Bw. Ahmada
amesema asilimia 5 ya mapato kwa ajili ya kuwawezesha vijana inaandaliwa ni
kuwa kichocheo cha maendeleo.
Wilaya ya Tanganyika bado ina
matatizo ya uhaba wa maji,waganga,wakunga na wauguzi,walimu katika shule za msingi
na sekondari huku miundombinu ya barabara nayo ikitakiwa kukarabatiwa.
Wilaya ya Tanganyika ina jumla ya
kata 16 ambapo miongoni mwa kata hizo ni pamoja na kata za Mishamo,Karema,Ipwaga,Ilangu,Bulamata,Mpanda
ndogo na makao makuu ya Wilaya ya Tanganyika kata ya Majalila.
Comments