LEO NI SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI MAADHIMISHO KITAIF AKUFANYIKA SHINYANGA,MIKOA 21 INAONGOZA KWA MIMBA ZA UTOTONI KINARA NI SHINYANGA KWA ASILIMIA 59.
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama
LEO ni siku ya mtoto wa kike duniani
ambapo siku hiyo kitaifa inaadhimishwa Mkoani Shinyanga.
Katika maadhimisho hayo yanayolenga
kuangazia matatizo yanayomkumba mtoto wa kike,Katibu mkuu wa Wizara ya
afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Sihaba Nkinga akiwa Wilayani
Kahama,ameitaka jamii kutambua haki za mtoto wa kike na kuwataka kutowaozesha
wakiwa chini ya umri mdogo.
‘’Bado changamoto moja inayokuta
mtoto wa kike ni ndoa na mimba za utoto ambayo kama taifa hatuwezi kukubaliana
nayo hatua nyingi tumefanaya lakini changamoto hii bado hatujaweza kuiondoa kabisa,tumeweza
kupunguza kwa kiasi lakini pia takwimu nyingine zimeendelea kutuonesha
kuwa miaka ijayo kutakuwa na watoto
wengi zaidi ambao watakatishwa ndotpo zao’’
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
anatarajiwa kuwa Mh.Ummy Mwalimu na kauli mbiyu mwaka huu ni “Mimba na Ndoa za Utotoni Zinaepukika:
Chukua Hatua Kumlinda Mtoto wa Kike’’
Takwimu zinaonesha mkoa wa Shinyanga
unaongoza kwa ndoa za utotoni, ukiwa na asilimia 59 ukifuatiwa na Tabora (58),
Mara (55), Dodoma (51), Lindi (48), Mbeya (45), Morogoro (42), Singida (52),
Rukwa (40), Ruvuma (39), Mwanza (37).
Mikoa mingine inayoongoza ni pmaoja
na, Kagera (36), Mtwara (35), Manyara (34), Pwani (33), Tanga (29), Arusha
(27), Kilimanjaro (27), Kigoma (29), Dar es Salaam (19) na Iringa (8).
Siku ya mtoto wa kike ilianzishwa rasmi na umoja wa mataifa mwaka 2012
Siku ya mtoto wa kike ilianzishwa rasmi na umoja wa mataifa mwaka 2012
Endelea kuwa name kufahamu kitakachojili kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments