SHIRIKA LA UNHCR LAKABIDHI GARI LA SHILINGI MILIONI 150 KWA JESHI LA POLISI WILAYANI TANGANYIKA,WAAHIDI KUTOA MAFUTA NA KULIKARABATI LINAPOHARIBIKA,JESHI LA POLISI KATAVI LAAGIZWA KUIMARISHA USALAMA.
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama- Katavi
SHIRIKA la Wakimbizi duniani UNHCR
limekabidhi gari mpya kwa jeshi la Polisi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,ili
kurahisisha na kuongeza utendaji kazi wa jeshi hilo katika kuimarisha usalama
wa raia na mali zao.
Akikabidhi gari hilo aina ya Toyota
Land Cruiser lenye thamani ya Shilingi Milioni 150,Mkuu wa Ofisi za Shirika la
UNHCR Wilayani Mpanda Bw.Deo
Rwasamanzi,amesema kuwa UNHCR wametoa gari hilo ili kuunga mkono juhudi
za serikali katika kurahisha usafiri kwa jeshi la Polisi ili kufanya kazi kwa
ufanisi katika kuimarisha usalama.
Aidha Bw. Rwasamanzi amesema shirika
la UNHCR litaendelea kutoa mafuta na ukarabati wa gari hilo na huduma nyingine
zinazohitajika ambapo hata hivyo ametoa wito kwa jeshi la polisi kulitumia
vizuri gari hilo ili lidumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Dkt Yahaya Hussein
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa niaba ya Katibu tawala mkoa wa Katavi
Kamishna Paul Chagonja ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya
makabidhiano ya gari hilo ambayo yamefanyika katika Ofisi za UNHCR zilizopo katika kata ya Mishamo ,ameliagiza
Jeshi la polisi kuhakikisha usalama unaimarishwa ikiwa ni sambamba na matumizi
sahihi ya gari hilo.
Aidha Dk Hussein mbali na kulipongeza
Shirika la UNHCR kwa msaada huo pia ametoa wito kwa mashirika mengine kujitokeza
kuunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo na kuimarisha usalama.
Mkuu wa kituo cha Polisi Wilayani
Tanganyika Amon Charles Mimanta baada ya kukabidhiwa gari hilo amesema,gari
hilo litasadia jeshi la polisi kufika mahali ambapo walikuwa hawafiki kutokana
na upungufu wa magari.
Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi
Agosti mwaka huu pia walikabidhiwa gari la wagonjwa ambapo takribani Magari 5
yamekwishakabidhiwa kwa serikali ya Mkoa wa Katavi kutoka kwa Shirika la UNHCR.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi
na watumishi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa
Makazi Mishamo Bw.Joseph Hossea,Kamati za ulinzi na usalama Wilaya ya
Tanganyika na Mkoa ,baadhi ya watumishi
wa UNHCR na uongozi wa kata ya Mishamo.
Miongoni mwa uharifu ambao umekuwa
ukitajwa kutokea mara kwa mara katika Wilaya ya Tanganyika ni pamoja na wizi
mdogomdogo wa mali za raia.
Endelea kuhabrika zaidi kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments