KUHUSU KATAVI NA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI LEO OKTOBA 11,2016-P5 TANZANIA INAKUSOGEZEA
Na.Issack
Gerald Bathromeo Mashama-Katavi
ZAIDI ya makosa 100 ya unyanyasaji
kwa mtoto wa kike yameripotiwa katika kipindi cha miezi 9 iliyopita ikiwa ni
pamoja na makosa ya ubakaji,kutupa watoto,kuwapa mimba wanafunzi na kuwaachisha
masomo.
Takwimu hizi ni kwa mjibu wa Mkuu wa dawati la jinsia na watoto Mkoani Katavi Afande Thobias Lindege ambazo amezitoa leo.
Kwa mjibu wa takwimu za umoja wa Matifa tangu kuanzishwa kwa siku ya mtoto wa kike
duniani mwaka 2012,Tanzania inashika nafasi ya 3 kati ya nchi wanachama wa
umoja wa mataifa 193 ikiongoza kwa kuwa mimba za utotoni ambapo mara nyingine
huambatana na vifo kutokana na maumbile changa ya watoto walio chini ya umri wa
miaka 18.
Maadhimisho
ya siku ya mtoto wa kike duniani hufanyika kila mwaka Oktoba 11 ambapo kwa
Tanzania maadhimisho haya yamefanyika Mkoani Shinyanga mkoa unaoongoza kwa
mi,mba za utotoni kwa asilimia 59 ukifuatiwa na Tabora wenye asilimia 58.
Kauli
mbiyu mwaka huu ni “Mimba na Ndoa za Utotoni Zinaepukika: Chukua Hatua Kumlinda
Mtoto wa Kike’’
Endelea kuhabarika P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Endelea kuhabarika P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni
au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments