WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA SHAMBULIO.
Na.Gervas Boniventure-Mpanda
WATU watatu wamefikishwa katika
mahakama ya mwanzo Mjini Mpanda Mkoani Katavi
kwa kosa la kumshambulia Abdala hamissi kwa kumpiga na kumsababishia maumivu
makali.
Akisoma shitaka hilo mbele ya
mahakama hiyo,mwendesha mashitaka wa
mahakama ya mwanzo Bi.Elly neema, amewataja washitakiwa hao kuwa ni Ramadhani
hamisi na Mohamed mussa wakazi wa nsemulwa pamoja na Maneno shabani ambaye ni
mkazi wa mikocheni Mjini Mpanda.
Bi.Neema ameiambia mahakama kuwa,mnamo
Januar 14 mwaka huu saa moja asubuhi washitakiwa walimshambulia Abdala hamisi
kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali
Kutokana na shitaka hilo washitakiwa
wamekana shitaka dhidi yao na hakimu wa mahakama hiyo Bw.David Mbembela ameahirisha
kesi hiyo mpaka itakaposikilizwa tena machi 2 mwaka huu.
Comments