WANAFUNZI 523 KATI YA 930 WAFAULU MTIHANI MANISPAA YA MPANDA,130 MATOKEO YAO YAZUILIWA KWA KUSHINDWA KULIPA ADA
Na.Vumilia Abel-Mpanda
JUMLA
ya wanafunzi 523 kati ya 930 waliofanya mtihani wa taifa kidato cha nne katika
Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda wamefaulu.
Miongoni mwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015 katika shule ya Sekondari Mwangaza Manispaa ya Mpanda (PICHA NA Issack Gerald) |
Wanafunzi wa kike Mpanda waliohitimu mwaka 2015 |
Takwimu
ya ufaulu huo umetolewa na Bi. Eneliya lutungulu ambaye ni Afisa elimu idara ya elimu sekondari
Manispa ya Mpanda wakati akizungumza na Mpanda Radio kwa njia ya simu.
Hata
hivyo amesma kuwa matokeo ambayo yamepokelewa mpaka sasa ni ya wanafunzi 800
huku matokeo ya wanafunzi 130 yakizuiliwa kwa sababu ya kuchelewesha ada ya
mtihani huo.
Bi.Lutungulu
amesema kuwa ufaulu kwa mwaka 2015 umeshuka kwa asilimia 65.4 ukilinganisha na
ufaulu wa asilimia 69 kwa mwaka 2014.
Aidha
Bi. lutungulu ameitaka jamii kutowaachia majukumu ya kifamilia watoto wao kwa
kuwa ni moja ya chanzo kinachosababisha utoro wa rejareja na kupelekea matokeo
mabaya katika masomo yao na taifa kwa ujumla.
Comments