JELA MIEZI 4 KWA WIZI WA SIMU MBILI
Na.Gervas
Boniveture-Mpanda
Mahakama
ya mwanzo mjini Mpanda imemhukumu mtu
mmoja kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya shilingi laki moja baada ya
kupatikana na kosa la wizi wa simu mbili zenye
thamani ya shilingi laki mbili.
Akisoma
hukumu hiyo jana,Hakimu wa mahakama hiyo
Bw. Robert Nyando amemtaja mshitakiwa kuwa ni Abass Philemon (21) mkazi wa Kawajense mjini Mpanda
mkoani Katavi.
Mlalamikaji
Agnes Mahanga ameieleza mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 31 Januari mwaka huu saa 4
asubuhi mshtakiwa alifika nyumbani kwa
Agnes Mahanga wakawa wamekaa baadae mshitakiwa alimuomba cm kwa lengo la
kuiangalia,baada ya kumpa cm hiyo agnes alitaka kwenda dukani kununua mafuta ya
taa ndipo mshitakiwa akaomba amfatie hayo mafuta.
Mshtakiwa
alienda dukani huku akiwa na cm ya agnes mahanga aina ya vodaphone yenye
thamani ya sh laki moja na hamsini na cm ya shahidi wake aina ya Tecno yenye
thamani ya sh elfu hamsini BILA ya yeye
kufahamu,mshitakiwa hakurudi kutoka dukani ndipo agnes mahanga alipogumdua kuwa
mshitakiwa ameondoka na cm yake.
alipoanza
kumfatilia kwa kushirikiana na shahidi waliekuwa wamekaa nae pindi mshitakiwa
huyo anafika nyumban hapo lakini hakufanikiwa kumpata’
Ndipo
mlalamikaji alipotoa taarifa hiyo katika jeshi la polisi na kufanikiwa
kumkamata mshitakiwa huyo.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo Mshtakiwa amekiri kosa na mahakama hiyo kutoa hukumu ya
kifungo cha miezi minne au kulipa faini ya shilingi laki moja ili iwe fundisho
kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Comments