RIPOTI YA PILI BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI SANNY YA KANISA LA (KKKT) ILIYOPO MKOANI KATAVI KUTEKETEA KWA MOTO HII HAPA,TATHMINI YA AWALI MALI ZA SHILINGI MILIONI 8.97 ZILITKETEA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Shule
ya sekondari ya Sanny inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) imesema kuwa thamani ya awali ya mali za wanafunzi zilizoteketea kwa
moto katika bweni la wavulana ni Milioni nane laki tisa na sabini elfu.
Mwonekano wa Sehemu ya bweni la wavulana lililoteketea kwa moto Shule ya Sekondari Sanny Tarehe 11.02.2016 |
Tathmini
hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Shule hiyo Sister Anna Usiri wakati akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Ofisi kwake.
Sister
Usiri ametaja baadhi ya mali zilizoteketea kwa moto katika tukio lililo
Februari 11 mwaka huu kuwa ni pamoja na magodoro,vitanda na sare za wanafunzi.
Wakati
huo huo amesema kuwa tathmini ya tukio hilo itatolewa hivi karibuni baada ya
mahandisi kufanya uchunguzi na jingo lote lililoteketea.
Halikadhalika
mkuu wa huyo wa shule amesema kuwa huenda tatizo hilo lilitokana na kutokea kwa tetemeko lililosababisha nyaya za
umeme kugusana na kusababsha moto huo.
Hata
hivyo Jeshi la polisi Mkoani Katavi limesema kuwa bado linaendelea na uchunguzi
ili kubaini chanzo cha moto ulioteketeza bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 31.
Hata
hivyo mpaka sasa,hajapata msaada wowote kutoka kwa wadau zaidi ya Mkuu wa Mkoa
kuahidi magodoro saba kwa wanafunzi walio athilika lakini hajaona chochote.
Comments