MTOTO MWENYE MIAKA 4 ACHOMWA MOTO NA BABA YAKE MZAZI KWA TUHUMA YA KULA MBOGA YOTE AINA YA CHAINIZI,POLISI WAMTIA MBARONI KUFIKISHWA MAHAKAMANI MUDA WOWOTE.
Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Emmanuel Joseph (31) mkazi wa Kata ya Kazima Wilayani Mpanda Mkoani Katavi anashikiliwa
na Jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa tuhuma za kumchoma kwa moto mtoto wake
aitwaye George Emmanuel(04) akituhumiwa kula mboga aina ya Chainizi.
Mtoto wa miaka 4 aliyechomwa moto na baba yake baada ya kula mboga aina ya chainizi.(PICHA NA.Issack Gerald) |
Kamanda Msaidizi wa Jeshi la Polisi
Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed,alisema tukio hilo lilitokea mnamo
tarehe 20.02.2016 majira ya saa kumi na moja jioni maeneo ya Kazima Kichangani Kata ya Kawajense
Tarafa ya Kashaulili Wilaya ya Mpanda Mkoa wa katavi
ACP
Mohamed alisema kuwa mtoto huyo alichomwa moto vidole vyake vya mkono wa
kushoto na baba yake mzazi baada ya mtoto huyo kula mboga yote ya majani aina
ya chainizi.
Bw.Emmanuel Joseph aliachana
na mke wake Semsin Jahala tangu mwezi wa tatu mwaka jana na kumwacha na watoto
watatu.
Taarifa
ya kamanda imefafanua kuwa mtuhumiwa alipika ugali pamoja na mboga aina ya
chainizi ambapo walikula mchana pamoja na watoto wake na kisha kubakiza kwa
lengo la kula jioni ambapo baada ya kula aliondoka na kwenda kwenye majukumu
yake ya kila siku ya utafutaji. Aliporudi nyumbani majira ya saa kumi na moja
jioni kwa lengo la kuandaa chakula cha jioni ndipo alipobaini mtoto wake huyo amekula
mboga yote kitendo kilichopelekea kumpiga na kisha kumchoma moto vidole vyake vitatu
vya mkono wa kushoto.
Hata
hivyo Mtoto George Emmanuel amepelekwa
katika hospitali ya Wilaya Mpanda kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Mtuhumiwa
anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
anatoa wito kwa wazazi/walezi wenye tabia ya kuwanyanyasa watoto kwa namna
yoyote ile kuacha mara moja tabia hiyo na badala yake watimize majukumu yao kwa
kuwatimizia mahitaji yote ya msingi wanayopaswa kupatiwa watoto wao ikiwa ni
sambamba na kuepuka kujichukulia sheria mikononi.
Comments