WANUFAIKA NA TASSAF WAPONGEZA MRADI HUO WILAYANI MLELE
Na.Issack
Gerald-Mlele.
BAADHI
ya wakazi wa Ilunde na Isegenezya kata ya Inyonga wilayani Mlele Mkoani Katavi
wameupongeza mradi wa kunusuru kaya masikini tasaf kwa kuwawezesha kujikwamua kimaisha.
Wakizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA katika kijiji
cha Ilunde wamesema mpango huo umewawezesha kusomesha watoto wao na kupata baadhi
ya huduma nzuri tofauti na hapo awali ambapo mpango huo ulikuwa hauja wafikia.
Hata
hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuimarisha mfuko huo wa tasaf ili
kuzifikia kaya maskini katika maeneo mbalimbali katika mkoa wa katavi na mikoa
mingine iliypo nchini.
Kwa
upande wake mratibu wa tasaf wilayani mlele Lucas Kombe amewataka wananchi hao
kutumia fedha hizo kwa malengo yanayokusudiwa na mfuko huo ili kupunguza
umaskini katika kaya hizo.
Comments