MKUU WA MKOA WA RUKWA AAGIZA KUOANDOLEWA MAAFISA WANNE KITENGO CHA FORODHA MKOANI HUMO
MKUU
wa Mkoa wa Rukwa Magalula Ssaid Magula ameagiza kuondolewa mara moja kwa
maofisa wa vitengo vinne kutoka katika kituo cha forodha cha Kasesya mpakani
mwa nchi ya Zambia wilayani Kalambo mkoani humo kwa tuhuma za kushindwa
kutekeleza maadili ya utumishi wa umma.
Mkuu
huyo wa mkoa amefika kituoni hapo akiwa na ujumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa kufuatia kukamatwa kwa roli la zaidi ya tani 40 lililosheheni
magogo ya miti aina ya mkurungu uliopigwa marufuku kusafirishwa.
Magalula
amesema, dalili zinaonesha maafisa hao wanasaidizana na wafanyabiashara
wasiokuwa waaminifu kuhujumu uchumi wa nchi ambapo magogo hayo thamani yake
haijajulikana.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wiki moja kwa Ofisa Upelelezi Mkoani Rukwa (RCO) kukamilisha uchunguzi wa
tukio hilo na kumkabidhi matokeo yake.
Comments