VIJIJI 7 WILAYANI NSIMBO VYALIA NA MIUNDOMBINU MIBOVU YA BARABARA
Na.Issack Gerald-NSIMBO
ZAIDI ya vijiji saba katika
Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi vinakabiliwa na ubovu wa miundombinu
ya barabara inayounganisha kijiji kimoja na kingine.
Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA baadhi ya
wakazi wa maeneo hayo akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Mnyaki B Bw. Justo
Sambayendi ametaja maeneo yenye miundombinu mibovu ni pamoja na ya barabara ya
kutoka Mnyaki kwenda Kabulonge,nduwi kwenda Iwimbi na Nduwi kwenda Kambuzi na
Mnyaki kwenda Kaminula.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Michael Nzyungu amekiri kuwepo kwa
changamoto hiyo na kuahidi ifikapo mwaka
ujao litafanyiwa utaratibu.
Comments