KAYA 8537 KATAVI ZANUFAIKA NA MRADI WA TASAF
KAYA
8537 katika vijiji 80 kati vijiji 177
vilivyopo Mkoani Katavi zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini Mkoani Katavi.
Hayo
yamesemwa na Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskini Tasaf Mkoani Katavi
Ignass Kikwala wakati akizungumza na wananachi wanaonufaika na mpango huo
katika kijiji cha Ilunde Kata ya Inyonga Wilayani Mlele.
Naye Mratibu wa Tasaf Wilayani Mlele Lucas Kombe
amewataka wananchi hao kutumia fedha hizo kwa kujiletea maendeleo katika kaya
zao.
Nao
wananchi wanaonufaika na mpango huo wamesema tasaf imeleta mabadiliko makubwa
katika kaya zao.
Comments