CHANAGAMOTO ZAENDELEA KUIANDAMA SHULE YA MSINGI KAWANZIGE
Na.Issack Gerald-MPANDA.
SHULE ya Msingi Kawanzige iliyopo Manispaa
ya Mpanda Mkoani Katavi yenye jumla ya wanafunzi 663 inakabiliwa na upungufu wa
madarasa ya wanafunzi pamoja na ofisi za Walimu.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Shuleni hapo,Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya
Msingi Kawanzige Ajaye Patrick amesema Wanafunzi hubadilishana madarasa wakati
wa kusoma kwa muda hali inayosababisha usumbufu kwa wanafunzi.
Mwalimu huyo ameiomba Serikali kujenga madarasa na ofisi za walimu,
huku akisema kuwa wazazi na wanafaunzi wameonesha ushirikiano mkubwa katika
kujenga shule hiyo hususani ufyatuaji wa tofali.
Sambamaba na Changamoto zinazoikabili
shule hiyo bado inafanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa ambapo mwaka jana
ilikuwa ya kwanza kati ya Shule 26 zilizopo Manispaa ya Mpanda ambapo kwa mwaka huu imeshika nafasi ya nne ikiwa na ufaulu wa asilimia 100.
Comments