WANAWAKE KATAVI WAASWA KUTOA TAARIFA ZA UKATIRI
Na.Issack Gerald-MPANDA.
WANAWAKE
Mkoani Katavi wametakiwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinavyojitokeza
katika familia na jamii kwa ujumla.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA,Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Faraja na Urafiki kwa Wanandoa na Ushauri kwa Vijana (FUNUVI)
Bi.Neema Kidima amesema asilimia kubwa
ya vitendo vya kikatili katika jamii unawakumba wanawake.
Aidha,mwitikio wa wanawake kutoa taarifa za
vitendo vya kikatili umekuwa kubwa changamoto
kutokana na mila na desturi zilizopo katika jamii.
Taifa
limeadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia
kuanzia oct 25 mwaka huu ambapo kilele chake
kimeafanyika jana desemba 10, huku Mkoani Katavi kilele kikifanyika
katika viwanja vya jeshi la polisi Mpanda.
Comments