MADIWANI NSIMBO WATAKIWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Na.Issack Gerald-NSIMBO
Baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya
ya Nsimbo Mkoani Katavi, limetakiwa kusimamia kikamilifu shughuli za maendeleo
katika kata zao pamoja na kutunza siri za serikali.
Wito huo umetolewa leo
na Mkuu wa wilaya ya Mlele kanali mstaafu Issa Suleiman Njiku katika zoezi la
kuwaapisha madiwani hao katika ukumbi wa halmashauri wilaya ya Nsimbo.
Kanali Njiku amesema
diwani anapaswa kusimamia miradi mbalimbali
pamoja na kusimamia hifadhi na mapori tengefu, ili kuzilinda maliasili
kwa ustawi wa taifa la Tanzania.
Aidha madiwani hao
baada ya kuapishwa wameteua kamati mbalimbali zitakazosimamia maendeleo katika
halmashauri hiyo, pamoja na kumchagua diwani wa kata ya Machimboni Bw. Raphael
Kalinga kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Comments