MADIWANI MPANDA WATAKIWA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI
Na.Issack Gerald-MPANDA.
MADIWANI wanaounda
baraza la madiwani halmashauri wa
wilaya ya mpanda walioapishwa leo wametakiwa kuanza kazi kwa kuzingatia maadili
na kuacha kufuata itikadi ya vyama vyao ili kuleta maendeleo ya wananchi
kwaujumla.
Hayo
yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi katika ukumbi wa
idara ya maji katika zoezi la kuwapisha madiwani hao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Pazza Mwamlima amewataka madiwani hao
kufanya kazi walizoagizwa na wananchi na kutatua changamoto zilizopo katika
kata zao ikiwemo elimu na afya.
Nao
baadhi ya madiwani walioapishwa wamesema watafanya kazi kwa kuzingatia sheria
na taratibu zilizowekwa, na kufuata kasi aliyoanza nayo Rais wa serikali ya
awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli.
Comments