ASKARI 38 WA WANYAMA PORI WATUNUKIWA VYETI KATAVI
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Jumla
ya wahitimu 38 walioshiriki mafunzo awamu ya pili ya Kijeshi katika Hifadhi ya
Wanyama pori Katavi, wametunukiwa vyeti katika madaraja mbalimbali.
Akifunga
mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa hifadhi za taifa Nchini Bw. Matongo Mtahiko
amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha nidhamu ya kuwawezesha
wahitimu kujua matumizi sahihi ya silaha.
Aidha
Bw. Mtahiko amesema mafunzo hayo ni maandalizi ya shirika la hifadhi Nchini
kutoka katika mfumo wa kiraia kwenda katika mfumo wa jeshi Usu.
Katika
mafunzo hayo idadi ya wanawake waliohitimu ni wanane wakati wanaume ni thelathini.
Comments