HAKI ZA BINADAMU WACHARUKA KUHUSU UKATIRI UNAOENDELEA MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa
kuripoti matukio ya ukiukwaji wa haki za
binadamu katika Ofisi za haki za binadamu wanapoona mamlaka husika Mkoani hapa
zinawanyanyasa katika haki zao mbalimbali.
Unapozungumzia haki za
binadamu,unakuwa unazungumzia kuhakikisha kuwa haki za msingi kwa binadamu
zinapatikana kwa haki tena ikiwezekana kwa mjibu wa sheria.
Siku ya haki za binadamu ilianzia
nchini Marekani wakati waafrika weusi nchini Humo walipokuwa wakidai haki zao
ili kujikomboa kutoka katika minyororo ya wazungu ambapo pia mbali na Afrika
pia hata Nchi ya Waisreal walipokuwa wamfungwa kule marekani walifanya hivyo
ili kunijinasua na matukio kandamizi.
Miongoni mwa haki za binadamu ni
pamoja nahaki ya kuishi.Lakini kwa mara kadhaa tuhuma mbalimbali zimekuwa
zikisikika maeneo mbalimbali ya dunia kuwa uvunjifu wa haki za binadamu
umekithiri ambapo mashirika kama Amnesty International yanayotetea haki mbali
mbalimbali za binadamu yamekuwa yakiingilia kati yanapogundua viashiria au
vitendo vya uvunjifu wa amani.
Katika kuangazia siku ya haki za
binadamu inayoadhimishwa kila ifikapo Desema 10,nimemtafuta Stanslaus Michael
Kisesa Mratibu wa Haki za Binadamu Mkoani
Katavi na Ukanda wa Mikoa ya Magharibi kwa ujumla ambapo katika mahojiano na P5 TANZANIA MEDIA pamoja na mabo
mengine amesema kuwa Wananchi Mkoani Katavi wanatakiwa kuripoti matukio ya
ukiukwaji wa haki za binadamu katika
Ofisi za haki za binadamu wanapoona mamlaka husika Mkoani Katavi zinawanyanyasa
katika haki zao mbalimbali pale ambapo wahusika kwa maana wanaotakiwa kutoa
huduma kwa mjibu wa sheria wanazikiuka maksudi kwa lengo la maslahi binafsi.
Florance Chareles ni mmoja wa wakazi waliopo mtaa wa Mpanda
Hotel Manispaa ya Mpana Mkoani Katavi kwa, upande wake akizungumzia siku ya
haki za binadamu ambapo pamoja na kuzungumza mengi anaona elimu bado haijatolewa
kwa kiasi cha kutosha kuwapelekea raia kutambua jinsi ya kupambana na viashiria
vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Sekta mbalimbali zikiwemo za ardhi na
maliasili zimekuwa zikitajwa na wananchi Mkoani Katavi zikihusishwa na matukio
au vitendo vya unyanyasaji kwa baadhi ya watu wakati mwingine hadi kupelekea
vifo.
Aidha mratibu wa haki za binadamu
Mkoani Katavi na Ukanda wa Magharibi kwa ujumla unaojumisha mikoa ya
Rukwa,Katavi,Kigoma na Tabora anazungtumzia ametaja idara ambazo wamekuwa wakizishughulika
nazo katika utatuzi wa matatizo ya wananchi hususani katika idara ya ardhi Manispaa
ya Mpanda ambapo amesema wamefanikiwa
kuwaelekeza hatua za kisheria katika kudai haki yao na hatimaye kupata haki yao.
Naye Emmanuel Mgiuna kwa upande
wake,ni mwanafunzi wa anayesomea sheria ya haki za Binadamu Mkoani Katavi amewaomba
wakurugenzi katika Halmashauri za Wilaya Mkoani Katavi kuhakikisha wanazingatia
sheria ili kila raia apate haki yake katika masuala mbalimbali kwa mjibu wa
sheria.
Hata hivyo Kisesa ametoa wito kwa
watumishi wa umma,na waliopo katika vitengo vya sheria wakiwemo mawakiri
binafsi kutojihusisha vitendo vya kutoa na kupokea na rushwa na badala yake
watende haki kwa kila raia kama sheria zinavyoelekeza katika mambo wanayoyahitaji
raia.
Baadhi ya maeneo ambayo wakazi
wamekuwa wakilalamika kudai haki zao ni pamoja na Kijiji cha Luhafwe ambako inaadiwa
mwaka 2013 kulitokea ukiukaji wa haki za binadamu ambapo mpaka leo wananchi
hawajafahamu uhalali wa kijiji chao kuwepo licha ya kuwa na huduma za jamii
ikiwemo shule.
Maeneo mengine ni pamoja na
Sitalike Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
ambapo wananchi wamekuwa wakidai kupigwa na askari wa wanayama pori mara kadhaa
wananchi wakitumiwa kuvamia hifadhi ya Taifa ya Wanyama Katavi lakini pia suala
la viwanja hususani Maeneo ya Mtaa wa Nsemulwa kata ya Nsemulwa Manispaa ya
Mpanda likionekana kuwa sugu kwa kushindikana kupatiwa ufumbuzi wa kutosha
tangu mwaka 2013.
Comments