WANANCHI KATAVI WAIOMBA SERIKALI YA AWAMU YA TANO CHINI YA MAGUFULI KUUNDA MAHAKAMA YA KIFAMILIA
Na.Agness
Mnubi-MPANDA.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya tano Ya Dk. John Pombe Maghufuli imeombwa kuunda Mahakama ya Kifamilia
itakayojihusisha na kushughulikia
vitendo vya ukatili na unyayasaji wa kijinsia.
Ombi
hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia inayofahamika kama Faraja
na Urafiki kwa Wanandoa na Ushauri kwa
Vijana(FUNUVI ) Bi.Neema Kidima Mkoani
Katavi,wakati akizungumza na P5 TANZANIA
MEDIA na mpanda redio juu ya mikakati ya kutokomeza vitendo vya ukatili
katika familia,jamii na Taifa kiujmla kwa mwaka 2016.
Amependekeza
kuwa mahakama hiyo iendeshwe na
wasimamizi wa kisheria na iwapo kesi ikishindikana mahakamani hapo ipelekwe katika ngazi za juu za kisheria.
Bi.
Kidima amefafanua kuwa kuundwa kwa Mahakama ya kifamilia, vitendo vya ukatili
na unyanayasaji wa kijinsia vinavyojitokeza vitashughulikiwa kwa ukaribu zaidi
kuliko ilivyo sasa ambapo idara inayoshughulika na masuala ya ukatiri kwa
watoto huchelewa kuyafanyia maamuzi kutokana na kuwa wanashuhulikia masuala
mengine ambayo yanakuwa yameletwa katika ofisi hizo.
Comments