BREAKING NEWS : MTOTO (16) ALALA NJE TANGU UTOTONI CHANZO WAZAZI KUMFUKUZA NYUMBANI,TAASISI ZA KUPINGA UNYANYASAJI ZAINGILIA KATI.
Na.Agness
Mnubi-MPANDA.
MTOTO anayefahamika kwa jina la Adamu
Ramadhan mkazi wa Manispaa ya Mpanda, yuko katika hatari ya kuathirika
kisaikolojia kutokana na vitendo vya kikatili.
Asasi ya FUNUVI inayohusika na faraja
kwa Wanandoa na Vijana mkoani Katavi katika barua yake yenye kumb.Na FUNUVI/MPD/MND/1/015
imekiri kupokea malalamiko ya kijana huyo.
Kijana
huyo (takribani miaka 16) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule
ya sekondari Kashaulili amefukuzwa nyumbani na wazazi wake jana
na kusababisha aishi maisha ya hatari.
Akihojiwa
na P5 TANZANIA MEDIA sanjari na Mpanda
Radio ,mtoto huyo amekiri kufanyiwa ukatiri na ikiwemo kupigwa na mama yake wa
kambo.
Juhudi
za kuwapata wazazi na maafisa wa ustawi wa jamii na jeshi la polisi kitengo cha
dawati la jinsia na watoto zinaendelea.
Comments