MTAFARUKU BAINA YA MANESI NA WANANCHI WANAOHITAJI HUDUMA HOSPITALINI MLELE.
Na.Suzan Kanenka-Mlele
Upungufu wa Manesi(wauguzi) katika
kitengo cha huduma ya afya ya uzazi katika hospitali ya Wilaya ya Mlele Mkoani
Katavi,umezua mtafaruku baina ya wahudumu wa kitengo hicho na wananchi
wanaostahili huduma hiyo.
Mtafaruku huo umetokea jana majira ya saa tano asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Mlele kutokan na idadi kubwa ya akina mama ambayo ilijitokeza kupata matibabu kuzidi kiwango kitendo ambacho kilisababisha wananchi hao kuanza kulalamika wakidai kuwa hawapati huduma kwa wakati.
Muuguzi aliyekuwa akitibu wagonjwa
katika hospitali hiyo Bi.Matha amesema kuwa kilichosababisha kutokea kwa vurugu
ni kutokana na mlundikano wa akina mama na watoto.
Aida amesema kuwa mlundikano wa kazi
alizokuwa nazo pia zimechangia kusababisha kutokea kwa mtafaruku huo.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa
Hospitali ya Wilaya ya Mlele Bi.Lucy Kafumu amekiri kupokea taarifa hiyo ambapo
amesema kuwa hali hiyo imetokana na upungufu wa watumishi katika hospitali hiyo
ambapo ameiomba serikali kuongeza nguvu zaidi katika kuajiri watumishi wa
kutosha katika Halmsahauri zilizopo pemezoni mwa mji.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ina
jumla ya zahanati 21 vituo vya afya 3,amabpo vinahitaji watumishi wapatao
305 huku walipo wakiwa 170 wakati huo
watu 154,000 ambapo watumishi wanaohitajika wakiwa 205.
Comments