UKAMATWAJI NYARA ZA SERIKALI KATAVI WAKITHIRI,WENGINE WAWILI WADAKWA NA KUSHIKILIWA NA POLISI,BAADHI YA WAKAZI KATAVI WATOA YA MOYONI.
Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi
Jeshi la polisi Mkoani
Katavi,linawashikilia watu watatu baada ya kukamatwa wakiwa na vipande 12 vya
meno ya tembo vikiwa na uzito wa kilogramu 11 ambapo thamani yake ni shilingi Milioni miamoja na
ishirini(120,000,000).
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa jana 29.12.2015 majira ya saa 4:00
usiku huko mtaa wa Airtel kata ya Uwanja
wa ndege tarafa ya Kashaulili Wilaya ya Mpanda.
Amewataja waliokamatwa kuwa ni Bathromeo
Augustino (26) mkazi wa Uwanja wa ndege,Geofrey Exavery (40) mkazi wa Uwanja wa
ndege na Elias Mwelala (42) mkazi wa makanyagio.
Kamanda Kidavashari,amesema kuwa kukamatwa kwa watu hao, kumetokana na
taarifa za raia wema kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kubainisha waharifiu
walipo na hatimaye kuwatia mikonnoni mwa polisi.
Watuhumiwa wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa hatua za
upelelezi na wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi anaendelea kuwaonya wananchi kuachana na biashara
haramu za nyara na uwindaji wa wanyama pori kwani ni uhalibifu wa rasilimali za Taifa na mazingira kwa ujumla.
Aidha, hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wote wasiotii sheria.
Hata hivyo baadhi ya wakazi
Mkoani Katavi wamesema kuwa kuna haja ya kuchunguza wasimamizi wa hifadhi nchini
kwani hakuna nyara za serikali zinazoweza kupatikana na kuelekea hatua ya
kuuzwa bila wao kufahamu.
Comments