VIKUNDI 14 VYA WAJASILIAMALI 60 MPANDA WAKOPESHWA MILIONI 27
Na.Agness Mnubi-MPANDA.
WAJASIRIAMALI 60
sawa na vikundi 14 kutoka Wilayani
Mpanda na Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamepata mkopo wa sh. Million 27
kupitia Mfuko wa Wajasiriamali Mpanda(METF).
Akikabidhi hundi za mikopo kwa
wajasiriamali hao katika ukumbi wa kanisa
katoliki leo, Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, katibu tawala Bw.
Donald Nkoswe Nkoswe amewataka kutumia fedha hizo kwa usahihi na kurudisha ili
ziwanufaishe na watu wengine.
Katibu wa Mfuko huo wa Wajasiriamali Mpanda Bi. Zena Kapama amewataka kutumia fedha hizo kwa usahihi ili kukuza
mitaji ya biashara zao, na kuweza kulipa
riba kwani wanarejesha kila mwezi kwa
riba ya asilimia 15 kwa mwaka
Mfuko wa wajasiriamali Mpanda ulianzishwa
tareher 4/1/2009 na aliyekuwa waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania MIZENGO
PINDA kwa kuwakutanisha wafanyabiashara
kwa lengo la kuanzisha mfuko ambao utawawezesha wajasiriamali wadogo kukopa kwa masharti na kwa riba nafuu.
Comments