JESHI LA POLISI KATAVI LAANZA KUTOA TAHADHARI MSIMU WA SIKUKUU 2015
Na.Issack Gerald-Katavi
Wakazi
Katika Mkoa wa Katavi wametakiwa kuepukana na Mazingira hatarishi Katika
kipindi hiki cha kuelekea Kipindi cha sikuku za Krismasi na mwaka mpya.
Kauli
hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa ACP Zahir Kidashavari katika taarifa
yake kwa vyombo vy habari kuhusu mikakati ya jeshi la polisi Kuimarisha usalama
Katika Kipindi cha sikukuu.
Katika taarifa yake ACP Kidavashari amesema
uzoefu unaonyesha kuwa Matukio mengi ya uhalifu ikiwemo wizi na ulevi wa
kupindukia hujitokeza na hivyo kuwataka wananchi wote kuchukua tahadhari.
Aidha
Kamanda Kidavashari
amewashukuru wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kwa kuonesha imani na kushirikiana
na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha Mkoa wa Katavi unaendelea kuwa salama
dhidi ya vitendo vinavyozorotesha ustawi wa amani na utulivu.
Comments