KAMATI ELIMU JUMUISHI MPANDA KUFANYA KIKAO LEO
Na.Issack Gerald-MPANDA
Kamati
ya kushughulikia elumu jumuishi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,leo wanatarajia
kukutana na wadau wa elimu hiyo kujadili masuala mbalimbali.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA Mratibu wa
elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael Fortunatus,amesema kikao hicho
kinatarajia kufanyika katika ofisi za Elimu Jumuishi zilizopo Manispaa ya
Mkoani Katavi.
Licha
ya kutobainisha mambo yatakayojadiliwa katika kikoa hicho,mambo ambayo yamekuwa
jakijadiliwa kupitia vikao kama hivyo ni pamoja na namna ya kumwezesha mtoto
aliyeko mazingira magumu kupata haki sawa kama watoto wengine hususani sekta ya
elimu.
Kmati
ya elimu Jumuishi Wilayani Mpanda inaundwa na idara mbalimbali zikiwemo asasi za kidini na binafsi huku katika vyombo
vya habari mwakilishi katika kamati hiyo akitokea Mpanda Radio fm.
Comments