SERIKALI YA TANZANIA KUZIMA SIMU BANDIA IFIKAPO JUNI,2016
Na.Katibu Mkuu Kiongozi-DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu kiongozi
Omben Sefue kwa kushirikaana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imetoa
tamko rasmi kuwa simu zote mkononi zisizo
halali yaani Bandia zitafungwa kutmumika ifikapo mwezi juni mwaka 2016.
Sefue amesema kuwa
lengo la kufunga matumizi ya simu hizo ni kudhibiti matukio ya uhalifu ya
kutumia simu zisizotambulika kwa urahisi na mitambo ya TCRA.
Amesema kuwa ili
kutambua uhalali wa simu yako unatakiwa kupiga *#06# ambapo utaona (IMEI namba)
ambapo utatakiwa kunakili namba hizo na kuzituma katika ujumbe mfupi kwenda
nambari 15090.
Hata hivyo,amesema kuwa ikiwa IMEI namba
haitaleta Jina la simu unatakiwa kurudisha kwa muuzaji au kubadilisha simu.
Comments