WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMA YA WILAYA MPANDA KWA VITENDO VYA RUSHWA
Na.Theressia
Lwanji-Mpanda Katavi
WATU Wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda
kwa kosa la Kujihusisha na Vitendo Vya kutoa na Kupokea Rushwa Kinyume
cha Sheria.
AKizungumza namtandao huu Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na
Rushwa Mkoani Katavi CHRISTOPHER NAKUA amesema Kwa Kipindi cha Kuanzia Mwezi
January Mpaka June Mwaka huu Takukuru imewafikisha watu wawili Mahakamani huku
Kesi nyigine zikiendelea Kuchunguzwa.
Katika hatua nyingine NAKUA ameitaka jamii kushirikiana na
Takukuru kwa kutoa taarifa za Watu wanaojihusisha na Vitendo vya Rushwa kwa
Vyombo vya Usalama ili Sheria ichukuliwe dhidi yao.
Hata hivyo takukuru imekuwa ikishauliwa na wadau wa masuala mbalimbali ya kijamii kuwa makini kufuatilia matukio yanayopekea kuwepo kwa vitendo vya rushwa Mkoani Katavi hususasni
kipindi cha uchaguzi ujao wa udiwani,ubunge na urais.
Comments