NSIMBO YAANZA MAANDALIZI SIKUKUU ZA NANENANE KITAIFA,UWANJA UTAKAOTUMIA WAWA CHANGAMOTO
Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imeanza maandalizi ya sikukuu ya Wakulima nane
nane huku ikikabiliwa na changamoto ya uwanja kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo Bw. Michael Nzyungu amesema hayo wakati akizungumza na
Mpanda Radio Ofisini kwake.
Amesema Nsimbo
inatarajia kuadhimisha sherehe za nanenane mwezi ujao mwaka huu kufuatia
waratibu wa sherehe hiyo kikanda ngazi ya taifa kuwataka kufanya hivyo.
Aidha amesema
kuwa ili sherehe zifanyike kwa ufanisi, inahitajika fedha ya kutosha ambapo
suala hilo limewasilishwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kufanikisha shughuli
hiyo.
Sikukuu ya
wakulima nanenane huadhimishwa kila mwaka Agosti nane ambapo maadhimisho hayo
kitaifa mwaka jana yalifanyika Mkoani Lindi.
Comments