RAIS KIKWETE AVUNJA BUNGE,AELEZA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KIPINDI CHA UONGOZI WAKE
Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kuainisha changamoto na mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika uongozi wake wa miaka 10 madarakani kabla ya kuagana na wabunge hao.
Pamoja na mambo mengine, Bunge hilo litakumbukwa kwa mjadala
mkali uliohusu maamuzi ya sakata ya uchotwaji wa zaidi ya shilingi bilioni 200
za akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa benki kuu ya Tanzania.
Sakata hiyo liliwaondoa mawaziri wawili na katibu mkuu wa
wizara ya nishati na madini na vigogo wengine wa Ikulu ya rais.
Hata hivyo hotuba yake imesusiwa na idadi kubwa ya wabunge wa
upinzani baada ya kulisusia bunge hilo kwa madai ya kupitisha miswada kadhaa
bila kufuata utaratibu amabapo pia wabunge kususia mikutano lilifanyika mwaka
2010 wakati Kikwete alipokuwa akilifungua bunge la kumi.
Hivi karibuni Wabunge wa upinzani walitangaza kususia vikao vya mwisho vya Bunge
hilo kutokana na uamuzi wa serikali kuwasilisha miswaada mitatu ya mafuta na
gesi kwa hati ya dharura hali iliyopelekea Spika wa Bunge Anna Makinda
kuahirisha bunge kwa muda usiojulikana ambapo hata hivyo aliwasimamisha baadhi
ya wabunge kushiriki baadhi ya vikao kwa mjibu wa kanuni za bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzania.
Comments