BALAZA LA MADIWANI MPANDA MJI LAMALIZA MUDA WAKE,KAMATI YA UKIMWI YAONGOZA MAPAMBANO YA UKIMWI
Na.Alinanuswe
Edward-Mpanda Katavi
BARAZA La Madiwani Katika halmashauri
ya Mji wa Mpanda jana limemaliza Muda wake wa Kipindi cha Miaka mitano ya kuwa
madarakani.
Katika kikao hicho Madiwani
wawakilisha wa kamati mbalimbali wamewasilisha taarifa zao ambapo Kamati ya Kupambana na Maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi ilyoko chini ya mwenyekiti Yusuphu Ngasa imefanya Vizuri
katika Kutoa elimu ya Kijikinga na Maambukizi ya Ukimwi.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa
Kikao hicho ambaye Pia ni Mwenyekiti wa
halmashauri ya Mji wa Mpanda iliyopanda hadhi ya nakuwa manispaa ya Mpanda
Enock Gwambasa amesema Mji wa Mpanda kuwa na Hadhi ya Manispaa itasaidia kuwepo
kwa Ushindani na Kuchochea uwajibikaji katika Idara zake utakaoleta Maendeleo kwa wananchi wake.
Kikao hiki cha mwisho ni Mkutano wa
Robo ya nne ya mwaka wa Fedha wa 2014/2015.
Comments