WALEMAVU MPANDA WAOMBA MAADHIMISHO KUFANYIKA NGAZI YA HALMASHAURI
NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi imesema inasubiri mwongozo wa serikali kuu ya Mkoa wa Katavi ili kuona
kama kuna uwezekano wa kuandaa maadhimisho siku ya walemavu duniani mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi
Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’a wakati akizungumza na
mtandao huu Ofisini kwake.
Ufafanuzi huo wa Mkurugenzi Chang’a unakuja
baada ya viongozi wa vyama vya walemavu Mkoani Katavi kuwasilisha barua kwa Mkurugenzi
wakiomba maadhimisho kufanyika ngazi ya Halmshauri wakati yanapokuwa
yakifanyika kitaifa katika mikoa mingine.
Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha
Walemavu wasioona Mkoani Katavi Issack Mlela hivi karibuni amesema,maadhimisho haya
yanayofanyika Oktoba kila mwaka yatafanyika mwezi Novemba mwaka huu Mkoani
Tabora baada ya kupisha Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba hapa nchini.
Maadhimisho haya yalifanyika mwaka
jana Mkoani Dodoma baada ya kuahirishwa kufanyika Mkoani Tabora kutokana na
Mkoa wa Dodoma kuwa nyuma katika kushughulikia masuala yanayohusu walemavu.
Comments