Posts

TMA WATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA LEO APRILI 13,2018

Image
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA imesema vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa leo Aprili 13,2018. Katika taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana Aprili 12,2018 mikoa ambayo inatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa ni Kagera,Geita, Mwanza,Mara, Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora,Katavi,Morogoro, Ruvuma,Dar Es Salaam, Pwani, Tanga Pamoja Na Visiwa Vya Unguja Na Pemba. Aidha TMA imetoa angalizo kwa kusema kuwa Vipindi Vifupi Vya Mvua Kubwa Vinatarajiwa Katika Baadhi Ya Maeneo Ya Mikoa Ya Rukwa, Njombe, Mbeya, Iringa Na Songwe. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RC KATAVI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KESHO JUMAMOSI APRILI 14,2018

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kesho siku ya Jumamosi Aprili 14,2018 ameitenga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya Mkoa wa Katavi kufika katika viwanja vya Azimio Mjini Mpanda kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi ili kueleza kero zao. Muhuga amesema atasikiliza kero za wananchi wote zinazohusu masuala mbalimbali na kuzipatia majibu papo hapo. Hii ni mara ya Kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga,kusikiliza kero za wananchi katika eneo la wazi linalojumuisha wananchi wote tangu alipoteuliwa mwaka 2016 kuwa Mkuu wa Mkoa kabla ya hapo amekuwa akisikiliza kero za wananchi Ofisini kwake. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RAIS MAGUFULI LEO APRILI 13,2018 KUWAVALISHA VYEO MAOFISA WA JWTZ AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE ANAYEREJESHWA JESHINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli leo Aprili 13,2018 anatarajia kuwavalishwa vyeo maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)   ambao amewapandisha vyeo jana Aprili 12,2018. Kati ya maofisa hao yumo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini. Kwa mjibu wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania , Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi. ORODHA YA WALIOPANDISHWA VYEO 1.Meja Jenerali Peter Massao aliyepandishwa kuwa Luteni Jenarali. 2.Brigedia Jenerali Henry Kamunde aliyepandishwa na kuwa meja jenerali. 3.D.D.M Mullugu 4.J.J Mwaseba 5.A.S Mwamy 6.R.K Kapinda 7.C.D Katenga 8.Z.S Kiwenge 9.M.A Mgambo 10.A.M Alphonce 11.A.P Mutta 12.A.V Chakila 13.M.G Mhagama 14.V.M Kisiri 15.C.E Msolla 16.S.M Mzee 17. C.J Ndiege 18.I.M Mhona 19.R.C Ng’umbi 20.S.J Mnkande ...

ZITTO ATAKA TAMISEMI IMTAFUTE MWENYEKITI WA HALAMSHAURI ALIYETOWEKA

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo),Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue. Amesema hayo bungeni jana Aprili 12,2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais,yenye wizara za Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019. “Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo,sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema. Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya. Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika. “Familia imechukua hatua mbalimbali,imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao,hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,”alisema Zitto.

RAIS AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo Aprili 12,2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) katika vyeo mbalimbali. Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo,Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.

WANANCHI KATAVI WATAKA VIONGOZI WA SERIKALI WAMUENZI SOKOINE KWA KUPELEKA HUDUMA MUHIMU ZA JAMII KWA WANANCHI

Wananchi Mkoani Katavi wamewashauri viongozi wa serikali wa serikali ya awamu ya tano kuenzi kifo cha Wazairi Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine kwa kupeleka huduma muhimu za kijamii kwa wananchi ikiwemo maji. Wakizungumza na P5TANZANIA kwa nyakati tofauti kuhusu kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha waziri mkuu hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki Apriki 12,1984 wamesema kuna maeneo mengi mkoani Katavi ambayo bado yanakosa huduma muhimu kama maji huku hata sehemu zenye zikipata kwa mgao. IAidha wametaka hata miradi ya maji iliyoanzishwa enzi za ukoloni ifufuliwe huku wakisema bado kuna hali ngumu ya kimaisha ambayo serikali inatakiwa iyatatue kama sehemu ya kumuenzi Sokoine. Aidha wamesema ni kiongozi aliyechukia uhujumu uchumi,rushwa,ufisadi huku akishiriki vema kuandaa majeshi wakatio wa vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda mwaka 1978. Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili Februaei 13 mwaka 1977 hadi Novemba 7 mwaka 1980 na   ...

RAIS MAGUFULI ATAKA WATANZANIA WAMUEZI SOKOINE KWA KUIGA MEMA ALIYOYAFANYA

Image
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli ametoa rai kwa watanzania kumuenzi Waziri Mkuu wa Zamani hayati Edward Moringe Sokoine kwa kujenga umoja,kupiga vita rushwa na kuchapa kazi. Rais ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia Aprili 12,1984 kwa ajali ya gari. Ajali hiyo ilitokea eneo la Dakawa nje Kidogo ya Mji wa Morogoro wakati akitokea Bumgeni Dodoma Kuelekea Jijini Dar es salaam. Amesema watanzania wanapoazimisha siku hii ya kifo chake, watanzania waige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa,mpiga vita rushwa,ufisadi,unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa. Rais amesema kwa upande wake anamkumbuka kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa la Tanzania na anasema alipata taarifa za kifo cha Sokoine   tarehe 12 Aprili 1984 akiwa Mpwapwa JKT nikitumikia...