Posts

MAOFISA WA JESHI LA POLISI 458 WATIMULIWA KAZI

Image
Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa jana Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha. Sirro alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza. Alifafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi. Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

POLISI RUKWA WAANZISHA OPARESHENI KUSAKA MASHAMBA YA BANGI.

Image
Jeshi la Polisi katika wilaya ya Kipolisi ya Raela Mkoani Rukwa limeanzishaa Oparesheni ya Kuyasaka mashamba yanayolima zao haramu ya bangi katika safu ya milima ya Lyamba Lyamfipa kwenye bonde la ziwa Rukwa. Mkuu wa Polisi katika wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela Mrakibu mwandamizi wa polisi Aloyce Nyantola akizungumza leo wakati akishuhudia vijana kutoka kata ya Kapenta wilayani Sumbawanga wakivuna shamba la bangi lenye ukubwa wa heka 2 amesema walipata taarifa za kilimo hicho kutoka kwa raia wema na ndipo walipoanza kuzifanyia kazi. Katika Oparesheni hizo Nyantola ametoa wito kwa wananchi kuwa wema kuendelea kutoa taarifa huku akiwtaka pia kuzingatia sheria za nchi   na kuachana na kilimo cha mazao haramu. Kwa upande wake mkuu wa upelelezi wa wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela mrakibu msaidizi Beda Msola amesema wananchi hao wamekuwa wakiendesha kilimo cha madawa ya kulevya ikiwemo bangi katika milima ya safu ya milima ya lyamba lyamfipa kwa kigezo kuwa maeneo ya msituni ...

RAIS MAGUFULI ASISITIZA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA DINI KULETA MAENDELEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya maendeleo hapa nchini. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika Ibada ya kumsimika Mhashamu Askofu Isaac Amani kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la MtakatifuTeresia wa Mtoto Yesu Jijini Arusha. Mhashamu Askofu Isaac Amani aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francis tarehe 27 Desemba,2017 kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo na amesimikwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski. Hatua ya rais Rais Magufuli kuhudhuria ibada hii ya kanisa katoliki imechukuliwa kama ishara bora ya kurejesha uhusiano mwema na baadhi ya makanisa makuu ya kikristo likiwemo kanisa katoliki ambao wamekua wakiikosoa vikali serikali yake....

AJALI YA BODABODA NA GARI KATAVI

Image
Dereva wa pikipiki maarufu kama Boda boda ambaye  jina lake halikufahamika Mara Moja Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,amejeruhiwa baada ya pikipiki yenye namba za usajil Mc 743 BQG aliyokuwa akiendesha kuligonga kwa Nyuma gari aina ya Raum eneo la Buzogwe njia mbili. Mashuhuda wa tukio hilo  ambalo limetokea leo wamesema,dereva huyo alikuwa akijaribu kuingia barabara kuu ya Buzogwe ndipo akawa amegongana na  Gari lenye namba za usajili T498 CFU.  Kwa mjibu wa mashuhuda hao,madereva wote wawili walikuwa na makosa baada ya wote kutozingatia sheria za usalama barabarani. Hata hivyo dereva wa gari hilo ambalo limegongana na pikpiki ametokomea kusikojulikana baada ya kutoonekana eneo la tukio baada ya Ajali hiyo kutokea. Hata hivyo askari polisi wa usalama barabarani ambao walifika eneo la tukio,wamekataa kuzungumzia tukio hilo wakidai wao siyo wasemaji. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

RAIS MAGUFULI ATOA SAA 24 KWA IGP AKIZINDUA NYUMBA 31 ZA POLISI

Image
Rais Dkt.John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP),Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho Aprili 8, 2018 awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo. Dkt.Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha. Amesema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto,huku akiwapongeza wadau mbalimbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo. Aidha amesema anataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo katika nyumba hizo ambapo ameeleza kuwa nyumba kuugua imedhihirisha makazi ya nyumba za polisi yalivyokuwa mabovu. Jumla ya nyumba 31 za polisi   mjini Arusha zimezinduliwa tayari kwa ajili ya polisi. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

DC AAGIZA WALIOKAIDI KUFANYA USAFI WAKAMTWE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wafanyabiasha wa soko la Buzogwe katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baada ya kukaidi agizo la kufanya usafi katika maeneo ya soko hilo. DC Lilian Matinga Picha na Issack Gerald Matinga ametoa agizo hilo leo wakati akishiriki zoezi la usafi katika soko la Buzogwe akiwa ameambatana na maafisa wa jeshi la polisi pamoja na watumishi wakiwemo watumishi wa umma. Amesema kuwa katika soko hilo hakuna aliyefanya usafi zadi ya mwenyekiti wa soko ambapo amesema watakaochukuliwa hatua watawajibishwa kwa kulipa faini ya shilingi 50,000 ikiwezekana hata kupelekwa mahabusu. Baadhi ya wananchi ambao wameshiriki zoezi la usafi wamesema kama serikali itaendelea kuhamasisha usafi mara kwa mara hakutakuwa na hofu ya magonjwa ya mlipuko. Jana mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,aliagiza watumishi wa umma na wananchi kushiriki katika zoezi la usafi kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 46 ya k...

KATAVI WAFANYA USAFI WAADHIMISHA KIFO CHA KARUME

Image
Serikali ya Mkoa wa Katavi umefanya zoezi la usafi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar   Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Katika taarifa iliyokuwa imetolewa jana na Afisa Habari wa Manispaa ya Mpanda Pius Donald alikuwa amebainisha maeneo yanayofanyiwa usafi kuwa ni pamoja na maeneo ya hospitali,sokoni na stendi kuu. Serikali imekuwa ikiwataka watanzania kufanya usafi wa hali ya juu katika maeneo yao ili kuendelea kuwa salama ikiwemo kuepuka maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama kipindipindu ambapo imekuwa ikifikia hatua ya kuchukua hatua kali za kisheria wa watu wanaokaidi kufanya usafi katika maeneo yao. Hayati Sheikh Abeid Amani Karume alizaliwa mwaka 1905 na alifariki dunia tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi hadaharani wakati akicheza bao huko Zanzibar. Habari zaidio ni  www.p5tanzania.blogspot.com