POLISI RUKWA WAANZISHA OPARESHENI KUSAKA MASHAMBA YA BANGI.
Jeshi la Polisi katika wilaya ya
Kipolisi ya Raela Mkoani Rukwa limeanzishaa Oparesheni ya Kuyasaka mashamba yanayolima
zao haramu ya bangi katika safu ya milima ya Lyamba Lyamfipa kwenye bonde la
ziwa Rukwa.
Mkuu wa Polisi katika wilaya hiyo ya
kipolisi ya Raela Mrakibu mwandamizi wa polisi Aloyce Nyantola akizungumza leo wakati
akishuhudia vijana kutoka kata ya Kapenta wilayani Sumbawanga wakivuna shamba
la bangi lenye ukubwa wa heka 2 amesema walipata taarifa za kilimo hicho kutoka kwa raia
wema na ndipo walipoanza kuzifanyia kazi.
Katika Oparesheni hizo Nyantola ametoa
wito kwa wananchi kuwa wema kuendelea kutoa taarifa huku akiwtaka pia kuzingatia
sheria za nchi na kuachana na kilimo cha
mazao haramu.
Kwa upande wake mkuu wa upelelezi wa
wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela mrakibu msaidizi Beda Msola amesema wananchi
hao wamekuwa wakiendesha kilimo cha madawa ya kulevya ikiwemo bangi katika
milima ya safu ya milima ya lyamba lyamfipa kwa kigezo kuwa maeneo ya msituni
hayafikiki kirahisi.
Miongoni mwa maeneo ambayo Oparesheni
imeanza leo ni pamoja na kata ya Ilemba,Kapenta na Kaoze kufuatia kilimo hicho
kushamiri katika maeneo hayo.
Hata hivyo Aprili 7 mwaka huu Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.John Magufuli akiwa ziarani Mkoani
Arusha,alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutofyeka mashamba ya
bangi badala yake watafutwe wahusika wa kilimo hicho ili hatua kali zichukuliwe
dhidi yao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments