Posts

JOKATE ATUMBULIWA UVCCM

Image
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyokutana kwa dharura mchana huu chini ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kheir Denis Jemes imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Jokate  U. Mwengelo kuanzia leo. Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.  Kikao hicho kilichomtengua Jokate kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.  Kheri Denis James (MCC) katika ukumbi wa secretariet  White house Mjini Dodoma lakini bado hawajaweka wazi sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo.  Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayan...

RAIS MAGUFULI KUPOKEA MAGARI 181 YA KUSAMBAZIA DAWA NCHINI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 yatakayokuwa yakitumika kusambaza madawa vijijini na mjini. Kwa mjibu wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt. Hassan Abbas Rais Magufuli ndiye atakuwa mgeni rasmi na kuzindua magari hayo 181. Magari hayo yapo chini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na yataongeza ufanisi katika kufikisha huduma katika maeneo yaliyokuwa hayafikiwi. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

UYOGA WAUA WAWILI KATAVI NA WENGINE MAHUTUTI

Image
Watu wawili ambao wametambulika kwa majina Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi wa kijiji cha   Stalike wilayani Mpanda mkoani Katavi,wafamefariki dunia baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na Sumu. Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher   Anjero amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo leo ambapo amesema mbali na marehemu hao,watu wengine watatu wako mahututi na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda. Bi.Monica George ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu amesema walikwenda porini kutafuta uyoga ambapo baada ya kupika na kula ndiyo wakapatwa na mauti hayo. Aidha George Anjero Mrisho amesema alipokea taarifa za kifo cha kijana wake Frenki Mayaga akiwa shambani. Hata hivyo Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda hakuupatikana ili kujua taratibu za kitabibu zinazoendelea kwa sababu hakuwepo kituoni. Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw. Christopher   Anjero hilo ni tukio la kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopit...

MAASKOFU WAANZA KUTEMA CHECHE SUALA LA KATIBA MPYA NA USALAMA WA TAIFA

Image
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk.Fredrick Shoo amesema kama taifa linahitaji maendeleo ya kweli basi kuna haja ya kuwa na katiba mpya na si iliyopo sasa.  Askofu Dk.Fredrick Shoo  Askofu Dk Fredrick Shoo alisema hayo baada ya kutoa ujumbe wa Pasaka na kusema kuna haja ya kuwa na katiba mpya ili kuweza kupata maendeleo ya kweli kwani katiba mpya ndiyo inaweza kuongoza kila raia.  "Katiba iongoze kila raia, utaratibu wa Watanzania kuweza kuishi pamoja na kama tunataka maendeleo ya kweli pasipo Katiba mpya tutakuwa tunajidanganya"  alisema Askofu Shoo  Mbali na hilo Askofu Shoo aliweza kuzungumzia mambo mengi kuhusu usalama wa nchi na watu wake na kuonyesha wasiwasi kuwa kuna vitu haviendi sawa kutokana na kuibuka kwa mambo ambayo si utamaduni wa Tanzania, kama watu kupigwa risasi, kuokotwa kwa miili ya watu baharini, kuuwawa kwa watu katika mazingira ya kutatanisha. Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM   ...

BARAZA LA MAASKOFU KUTEMA CHECHE KESHO KUHUSU HALI YA USALAMA WA TANZANIA NA WATU WAKE

Image
Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini. Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo. Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji,utesaji,kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa,mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi,vitisho, ubambikiziaji wa kesi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi. Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza,kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge,Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa. jumbe huu kutoka baraza la maaskofu wa KKKT umekuja siku chache tu baada...

KAULI YA WAZIRI ISIPOFAFANULIWA VIZURI INAWEZA KUSABABISHA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU SHULENI

Image
Miaka michache baada ya serikali yenyewe kufuta adhabu ya viboko shuleni,Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk.Mwigulu Nchemba,amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike. Waziri Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari   Lulumba Wilayani Iramba mkoani Singida ambapo amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi. Katika hatua nyingine amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa. Mbali na hayo Dk.Nchemba amesema majengo ya taasisi za serikali yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo. Imekuwa ikishuhudiwa baadhi ya walimu wakiwachapa wanafunzi mpaka kusababisha majeraha hata baadhi ya walimu hao kufukuzwa kazi,je,kauli ya Wazi...

SERIKALI YAFUNGUKA KUHUSU KUFUNGIA MITANDAO

Image
Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt.John Magufuli imekanusha taarifa ya kufungia mitandao ya kijamii kama inavyoelezwa na baadhi ya watu na kuitaka jamii kuzipuuza endapo watakutana nazo mitandaoni. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa asubuhi ya leo katika ukurasa wake maalumu wa kijamii na kusema taarifa hizo ni uzushi mtupu hazina ukweli wowote ambayo imetengenezwa na wahalifu wa mtandao. Leo (Machi 24, 2018) imesambazwa barua iliyokuwa inaonesha kutoka Ikulu ambayo imeandika taarifa za kuwa serikali inawaasa watanzania wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuitumia kwa uangalifu na tija ili kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com